Yanga kujipima na JKU

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2024
Yanga kujipima na JKU

Kikosi cha Yanga siku ya Jumamosi kinatarajiwa kucheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya JKU ya Zanzibar katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kwa ajili ya michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko Ivory Coast

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi aliwaagiza viongozi wa Yanga kuhakikisha wanapata angalau mechi mbili kila wiki ili kuhakikisha kikosi chake kinaendelea kubaki katika hali ya ushindani

Uongozi wa Yanga pia unatafuta timu nyingine kutoka nje ambayo itatoa upinzani unaoendana na mechi ambazo Yanga itakwenda kucheza pale michuano ya Afcon 2023 itakapomalizika

Gamondi amesema ni muhimu kwa vijana wake kupata mechi za kujipima nguvu ili kuona wamefanikiwa kwa kiasi gani katika maandalizi wanayoendelea nayo

"Tumerejea mapema kwenye mazoezi kuweza kujipanga kwa muda huu ambao upo kwa sasa, unajua tuna wachezaji wapya ambao wamesajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili, tupo nao kwenye mazoezi hivyo ni vizuri kupata michezo ya kirafiki kuangalia kikosi chetu"

"Tunalenga kuboresha timu yetu tukiwa na malengo ya kufanya vizuri kimataifa, michezo hii ya kirafiki baada ya kuongeza wachezaji itanipa picha ya nini napaswan kuongeza au kuboresha," amesema Gamondi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’