Bacca anaweza kucheza Ulaya - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2024
Bacca anaweza kucheza Ulaya - Zahera

Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amemwagia sifa beki wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Ibrahim Hamad 'Bacca' kwa kiwango bora anachoonyesha katika michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko Ivory Coast

Bacca amekuwa nguzo muhimu ya safu ya ulinzi ya Stars katika michuano hiyo akitumika katika mechi zote 2 dhidi ya Morocco na Zambia

Zahera ambaye kwa sasa anainoa Namungo Fc, amesema anafuatilia michuano hiyo na amevutiwa na uwezo unaoonyeshwa Bacca huku akibainisha kuwa ana sifa zote za kucheza soka barani Ulaya

"Nimetazama mechi mbili za Tanzania waliyocheza na Morocco na ile waliyocheza na Zambia"

"Nimemtizama yule beki wa Yanga anatokea Zanzibar (Bacca) ni mchezaji mzuri sana na anaweza kucheza soka Ulaya," alisema Zahera

Bacca ni mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri katika michuano hiyo akiwekwa katika orodha ya wachezaji waliopiga pasi nyingi zaidi akiwa na wastani wa kupiga pasi 64 kwa mchezo

Haitashangaza baada ya michuano hii ofa zikamiminika Jangwani kuitaka huduma yake

Bacca bado ana mkataba wa muda mrefu na Yanga kwani mwezi Disemba 2023 alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
20h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
21h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’