Mikwaju ya penati inavyoitesa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Apr 2018
Mikwaju ya penati inavyoitesa Yanga
Kwa miaka ya hivi karibuni Yanga imekosa ufanisi linapokuja swala la changamoto ya mikwaju ya penati.

Ni kama Yanga imekuwa na 'bahati ndogo' au haina bahati kabisa kila inapofika katika hatua hiyo.

Nakumbuka wakati wa michuano ya Sportpesa msimu uliopita Yanga iliondoshwa kwenye mashindano hayo kwa mikwaju ya penati na AFC Leopards.

Ikaja kufungwa na Simba kwa mikwaju ya penati mchezo wa Ngao ya Jamii.

Kombe la Mapinduzi, Yanga ikatupwa nje kwa mikwaju ya penati na URA.

Ikabahatisha kuiondoa Ihefu FC kwa mikwaju ya penati kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la FA.

Jana imerejea rekodi yake 'iliyozoea' kwa kuondoshwa na Singida United kwenye robo fainali ya michuano ya kombe la FA.

Yani kama ni ku-bet, odd za Yanga kwenye mikwaju ya penati zingekuwa ndogo sana kutokana na rekodi yake mbovu.

Bahati mbaya hakuna kocha wa kufundisha wachezaji kupiga mikwaju ya penati. Hili ni swala la kujiongeza kwa mchezaji mwenyewe.

Muhimu ni kwa benchi la ufundi kuwa na muda maalum kwa wachezaji kufanya mazoezi ya kupiga penati kila siku

Pia wachezaji wanapaswa waandaliwe kisaikolojia kabla ya kwenda kwenye matuta.

Kwa kuwa mara kwa mara Yanga imekuwa haifanyi vizuri inapokuja changamoto ya matuta, kwa wachezaji pia huenda imejengeka hofu kuwa 'hatuwezi'

Tatizo hili linasababisha wachezaji kukosa kujiamini na kujikuta wanakosa penati kwa urahisi.

Hapa haipaswi kuwalaumu wachezaji wanapokosa, jambo la msingi ni kuwapa moyo ili waweze kurekebisha makosa yao.

Kama tutaendelea na huu utamaduni wa kuwalaumu wachezaji wanapokosa penati basi tufahamu ipo siku timu haitakuwa na mpiga penati.

Wachezaji wote watalikwepa jukumu hilo ili kujiokoa na lawama.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’