Guede kutua wiki hii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jan 2024
Guede kutua wiki hii

Wiki hii mshambuliaji mpya wa Yanga Joseph Guede anatarajiwa kutua nchini kuungana na wenzake ambao wanaendelea na mazoezi Avic Town kujiandaa na mechi za Ligi Kuu, kombe la FA na Ligi ya Mabingwa

Baada ya kukamilisha usajili wake, Guede alipewa ruhusa maalum ili akamilishe masuala binafsi kabla ya kutua nchini kuanza majukumu mapya na mabingwa hao wa nchi

Yanga inarejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki ambapo wiki hii vijana wa Kocha Miguel Gamondi wanatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki

Katika moja ya mahojiano yake, Gamondi alisema amemuagiza Guede akatishe mapumziko na kutua nchini haraka ili aanze mazoezi na wenzake

Gamondi alisema Guede anatakiwa kuja kufanya maandalizi haraka na wenzake ambayo yatamrahisishia kuwa na mwanzo mzuri ndani ya timu hiyo wakati wa mashindano utakaporejea

"Tunaendelea na mazoezi yetu, wikiendi tulipumzika kidogo kazi zaidi itaendelea Jumatatu ni muhimu kuwa tayari mapema nafurahia jinsi wachezaji wanavyojituma licha ya ugumu wa ratiba ya mazoezi"

"Kwa sasa kila mchezaji ambaye hayupo na timu ya taifa tupo naye kasoro kijana wetu Guede. Nimeongea naye nimemwambia umuhimu wa kuwahi haraka kuja kuanza kazi"

"Anahitaji kuanzia hapa ambako tunafanya sasa ili imsaidie kuwa sawa na wenzake, naamini atafika kama ambavyo tumezungumza, hatuna shida sana na hawa ambao wako timu za taifa kwa kuwa wao wanapata mazoezi ya kutosha," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’