Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inatupa tiketi muhimu kwenye michuano ya Afcon 2023 inayoendelea huko Ivory Coast kwa mchezo dhidi ya Zambia
Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kubugizwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco, Tanzania leo inahtaji ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya 16 bora
Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi hasa ikizingatiwa hata Zambia wanazihitaji alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri
Zambia wana alama moja baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya DR Congo katika mchezo uliopita
Stars itaingia katika mchezo huo ikiongozwa na makocha wazawa Hemedy Morocco na Juma Mgunda baada ya aliyekuwa kocha Mkuu Adel Amrauche kusimamishwa na CAF na TFF kumpa mkono wa kwaheri huko huko Ivory Coast
Morocco na DR Congo ztachuana katika mchezo wa mapema utakaopigwa saa 11 jioni