Kamwe atamba, Guede ataongeza dozi Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jan 2024
Kamwe atamba, Guede ataongeza dozi Ligi Kuu

Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema ujio wa mshambuliaji Joseph Guede utakwenda kumaliza changamoto katika safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa Tanzania Bara

Yanga ilifunga dirisha dogo la usajili Januari 15 kwa utambulisho wa mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast aliyewahi kutamba na FAR Rabat, mabingwa wa Ligi Kuu ya Morocco

Kamwe ametamba kuwa Yanga haikukurupuka kumsajili Guede, walipata muda wa kumfuatilia na kujiridhisha kuwa anaweza kuwa mrithi wa Fiston Mayele aliyetimkia Pyramids Fc ya Misri

 Kamwe amesema baada ya subira ya muda mrefu, Wananchi sasa wamepata mtu sahihi wa kurithi nafasi ya Mayele

"Lilikuwa ni ombi la muda mrefu la mashabiki wetu kupata Mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kama ambavyo ilikuwa kwa Fiston Mayele na uongozi kupitia ripoti ya kocha mkuu Miguel Gamondi umemleta Guede"

"Nataka niwaambie, Guede ni mshambuliaji aliyekamilika, anafunga na kutoa pasi za mabao pia. Pamoja na vipigo tulivyokuwa tukitoa, malalamiko kuhusu safu yetu ya ushambuliaji yalikuwa mengi"

"Kupitia usajili huu nawaonya wapinzani wetu kuwa waandae safu zao za ulinzi vizuri la sivyo ile kasi ya kuwapiga watu magoli mengi itaongezeka maradufu," alitamba Kamwe

Guede anakuja kuwaongezea ushindani Clement Mzize na Kennedy Musonda ambaye uko katika majukumu ya timu ya Taifa ya Zambia inayoshiriki michuano ya Afcon 2023

Ni wazi wapinzani wanapaswa kujipanga kwelikweli kukabiliana na Yanga pale michuano mbalimbali itakaporejea baada ya kumalizika Afcon 2023

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’