Ukiwaangalia Ivory Coast wanavyocheza utajiuliza ilikuwaje kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua hakujumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha wenyejii hao wa michuano ya Afcon 2023
Jana Ivory Coast walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Nigeria na kuweka rehani hatma yao ya kutinga hatua ya 16 bora kwani watahitaji kupata ushindi mchezo wa mwisho dhidi ya Guinbea ya ikweta ambao ndio vinara wa kundi A
Pacome alijumuishwa katika kikosi cha awali lakini akondolewa kwenye mchujo wa mwisho uliobakisha wachezaji 27
Pacome amekuwa na msimu bora akiwa na Yanga, ndiye kinara wa mabao kwa Yanga kwenye ligi ya mabingwa akiwa na mabao matatu akizidiwa bao moja tu na Sankara Karamoko wa Asec Mimosas ambaye anaongoza kwa mabao katika michuano hiyo. Karamoko nae hakujumuishwa katika kikosi hicho
Pacome pia amepachika mabao manne katika ligi kuu ya NBC
Pengine Ivory Coast wangenufaika zaidi kama wangemjumuisha katika kikosi chao
Achilia mbali Pacome, hata Yao angeweza kuuwasha moto vilevile kama angeitwa katika kikosi hicho