Ubingwa sasa ni lazima kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Apr 2018
Ubingwa sasa ni lazima kwa Yanga
Baada ya kutolewa kwa matuta na Singida United kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA, Yanga sasa italazimika kutwaa ubingwa wa VPL kwa msimu wa nne mfululizo ili iweze kushiriki michuano ya Kimataifa mwakani.

Singida United imetumia faida ya kucheza nyumbani na kuibuka na ushindi wa penati 4-2 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1.

Yanga ikiwa na alama 46 sawa na Simba inayoshuka dimbani Jumanne kucheza mchezo wa kiporo dhidi ya Njombe Mji, haihitaji kufanya makosa mengi kwenye ligi ili iweze kuibuka mbele ya mahasimu wake.

Aidha matokeo haya yameongeza ushindani kwenye ligi baina ya Simba na Yanga na zaidi ukiwa mchezo baina yao utakaopigwa April 29, 2018.

Yanga bado ina nafasi muhimu ya kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika kama itaibuka na ushindi dhidi ya Welayta Dicha katika michezo yote miwili.

Itaanzia nyumbani kwenye uwanja wa Taifa April 07 kisha kwenda kumalizia nchini Ethiopia April 17.

Aidha baada ya mchezo dhidi ya Welayta Dicha April 07, Yanga itarejeana tena na Singida United April 11 safari hii ikiwa ni mchezo wa ligi utakaopigwa katika uwanja wa Taifa.

Huu utakuwa mchezo wa kisasi kwa vijana wa George Lwandamina.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’