Yanga yatolewa kwa matuta kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Apr 2018
Yanga yatolewa kwa matuta kombe la FA
Singida United imetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la FA (ASFC) baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya bao 1-1.

Radha ya mchezo huo ilivurugika tangu dakika ya kwanza baada ya mvua kubwa kunyesha na kuwapa wakati mgumu wachezaji katika umiliki wa mpira.

Yanga ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 23 mfungaji akiwa Yusuph Mhilu aliyeunganisha vyema kwa kichwa mpira wa kona uliokuwa umepigwa na Ibrahim Ajib.

Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Singida United ambayo ilikosa nafasi kadhaa za kufunga kwenye kipindi cha kwanza.

Singida United ilirejea mchezoni dakika mbili tu tangu kuanza kwa kipindi cha pili Kenny Ali akifunga bao safi ya kusawazisha baada ya mabeki wa Yanga kuzembea kuondoa mpira langoni kwao.

Licha ya mashambulizi ya hapa na pale kutoka kila upande, mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 na mshindi ikabidi apatikane kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Kelvin Yondani na Gadiel Michael walifunga penati za Yanga huku Papi Tshishimbi na Emanuel Martin wakikosa.

Kwa upande wa Singida United Batambuze, Kutinyu, Kenny na Sumbi walifunga penati zao huku Atiri akikosa.

Singida United sasa itachuana na JKT Tanzania kwenye mchezo wa nusu fainali wakati Stand United itakabiliana na Mtibwa Sugar.

Yanga sasa inalazimika kuhakikisha inatetea ubingwa wa VPL ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’