Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa kesho Jumatatu, Januari 15 2024 saa 5:59 usiku
Katika dirisha hili mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji wawili ambao ni Shekhan Khamis (JKU) na Augustine Okrah (Bechem United) huku ikimtoa kwa mkopo Crispine Ngushi kwenda klabu ya Coastal Union
Wananchi wanasubiri kwa hamu kuona Yanga inafungaje dirisha hili taarifa za ndani zikibainisha kuwa hesabu bado hazijakamilika
Maboresho ya safu ya ushambuliaji ndio yanayosubiriwa kwa hamu ili kuongeza nguvu eneo hilo
Baada ya kuondoshwa katika michuano ya kombe la Mapinduzi, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alibainisha kuwa michuano hiyo ilimsaidia kubaini mapungufu ya kikosi chake na aina ya maboresho ambayo aliyahitaji yafanyike
Aliwasilisha mapendekezo yake kwa uongozi wa Yanga na sasa ndani ya saa 24 itafahamika waliotoka na walioingia