Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika Eng.Hersi Ally Said amechangia Tsh millioni 10 na Tsh millioni 50 kutoka kwa mdhamini na mfadhili Ghalib Said Mohamed kwenye hafla ya Harambee ya kuchangia timu za Taifa iliyofanyika jana katika Hoteli ya Johari Rotana
Harambee hiyo iliongozwa na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa ambae alisema lengo ni kukusanya Sh bilioni 10 ambazo zitagawanywa kwa timu zote za Taifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan na rafiki zake walichangia Tsh milioni 500
Rais Samia akipiga simu kuchangia harambee hiyo alisema;
"Michezo ni jukumu letu, jukumu la serikali, jukumu la watanzania, serikali tumejitahidi sana kukuza michezo, serikali tumetoa vivutio timu zimetuitikia, " amesema na kuongeza
"Lakini tumefika mahali tuna uchache wa bajeti, nawaomba tuchangie ili timu zetu ziende kushindana na sio kushiriki, kwa kuanzia mimi na rafiki zangu tutatoa Sh milioni 500"
Jumla ya Tsh Bilioni 3.7 zilikusanywa katika Harambee hiyo