Waamuzi wavurunda kombe la Mapinduzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2024
Waamuzi wavurunda kombe la Mapinduzi

Mjadala mkubwa unaoendelea katika mitandao ya kijamii ni matukio ya yaliyojiri kwenye kombe la Mapinduzi kwa waamuzi kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za soka na hivyo kuzinufaisha timu ambazo hazikustahili

Pengine katika michuano ya mwaka huu ndio imeshuhudia makosa mengi yakifanywa na waamuzi kuliko wakati mwingine wowote tangu michuano hiyo ilipoanzishwa

Jana Kamati ya waamuzi ya michuano hiyo ilitangaza kumfungia mwamuzi wa kwanza msaidizi Yusuf Shombe Issa kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria kwa kuruhusu bao la kwanza la Azam na baadaye Singida Fountain Gate ambayo hayakuwa halali katika mchezo wa robo fainali

Azam iliandika bao la kwanza kupitia kwa Alassane Diao kwa kichwa akionekana ameotea kabla ya Singida kupata bao la pili lililofungwa na Habib Kyombo akionekana pia ameotea na kufanya matokeo ya mwisho Singida kushinda 2-1 na kutinga nusu fainali

Mbali na Issa, pia Shekha alisema mwamuzi wa pili aliyefungiwa ni Mohamed Mwadini aliyekuwa mwamuzi wa kwanza msaidizi ambaye aliruhusu bao katika mchezo wa makundi kati ya JKU na APR akidai mpira ulivuka mstari wa goli wakati haikuwa hivyo

Mechi hiyo iliisha kwa APR kushinda mabao 3-1 na kwenda robo fainali ambako ilifanikiwa kuiondosha Yanga kabla ya kutolewa na Mlandege katika nusu fainali

Jana katika mchezo wa nusu fainali kati ya Singida FG dhidi ya Simba madudu mengine yakafanyika Singida FG wakipoteza mchezo huo kupitia mikwaju ya penati

Licha ya kuongezwa dakika 6 baada ya dakika 90 kumalizika, mchezo ulichezwa kwa takribani dakika 100 Simba ikisawazisha bao katika dakika ya 9 kati ya 10 zilizochezwa kupitia mpira wa kona ambao ulikuwa na utata

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Waziri Shekha amesema baada ya kikao kilichofanyika leo Januari 11, 2024 kupitia ufanisi uliofanywa mwamuzi Msomali na wasaidizi wake wamegundua kwamba mwamuzi huyo hakuwa sahihi kwenye uamuzi wake huo wa kuwapa kona Simba ambayo ilizaa bao la kusawazisha

Shekha amesema kosa hilo ni la kibinadamu kwani waamuzi nao hufanya makosa..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’