Lwandamina atumia kikosi kilichoizuia Township Rollers kwao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2018
Lwandamina atumia kikosi kilichoizuia Township Rollers kwao
Leo Jumapili Yanga inashuka kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida kuivaa Singida United kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA (ASFC).

Tayari Yanga imeweka hadharani kikosi chake ambapo Kocha George Lwandamina 'Chicken' ametumia kikosi kilichotoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Township Rollers katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa nchini Botswana.

Mabadiliko pekee aliyofanya kwenye kikosi hicho ni kumuingiza Ibrahim Ajib nafasi ya Thabani Kamusoko.

Lwandamina amewapumzisha Kamusoko na Ngoma. Licha ya kuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri mkoani Singida, hawatacheza mchezo huo.

Ikumbukwe baada ya mchezo huu Yanga ina mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha April 07 kwenye uwanja wa Taifa.

Kocha Lwandamina na mlinda lango Ramadhani Kabwili wametua Singida asubuhi ya leo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’