Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kupoteza mchezo wa robo fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya APR hayakuwa malengo yao
Kamwe amesema watajipanga ili kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika michuano ijayo
Aidha Kamwe amesisitiza kuwa Yanga haikudharau mashindano hayo, kilichotokea ni sehemu ya matokeo ya mpira wa miguu
"Tulikuja Zanzibar kushindana na lengo letu lilikuwa kutwaa taji hili lakini imekuwa bahati mbaya tumepoteza mchezo wa robo fainali dhidi ya APR"
"Hatukudharau michuano hii kauli hizi zinatolewa sasa kwa sababu tumefungwa lakini hazikutolewa wakati tunashinda mabao matano katika hatua ya makundi"
"Lazima tuheshimu matokeo ya mpira wa miguu, tunawapongeza APR kwa ushindi waliopata sisi tutajipanga kwa ajili ya michuano ijayo," alisema Kamwe
Yanga inarejea jijini Dar es salaam leo kuendelea na ratiba nyingine