Mtibwa Sugar imekuwa timu ya tatu kutinga nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuiondosha Azam FC kwa mikwaju ya penati 9-8 kufuatia matokeo ya 0-0 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi.
Mtibwa Sugar imeungana na timu za Stand United na JKT Tanzania kutinga hatua hiyo.
Stand United iliichapa Njombe bao 1-0 wakati JKT Tanzania iliilaza Prisons mabao 2-0.
Mchezo wa kukamilisha timu nne za nusu fainali utapigwa kesho Jumapili ambapo Singida United itawakaribisha mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga katika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Namfua mkoani Singida.

ADVERTISE HERE