Yanga haikukurupuka kumsajili Augustine Okrah, ni mchezaji ambaye alikidhi vigezo na Kocha Miguel Gamondi kuridhia usajili wake
Okrah huyu aliyesajiliwa na Yanga sio yule aliyeitumikia Simba msimu mmoja
Okrah ametua timu ambayo haina zengwe, atakuwa na nafasi ya kuonyesha uwezo na thamani yake
Ukiangalia takwimu za Okrah katika misimu mitatu iliyopita akiwa katika timu za Simba na Bechem United, utakubali huyu ni mchezaji wa daraja la juu
Okrah amefunga takribani mabao 27 na kutoa assist 11, akiwa ni kiungo mshambuliaji
Jambo la uhakika Okrah atadhihirisha thamani yake akiwa na Yanga

Β
ADVERTISE HERE