Kikosi cha Yanga ambacho kiko visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi, kimewajumuisha wachezaji saba kutoka timu ya vijana U20
Vijana waliojumuishwa katika kikosi hicho ni Awesu Kassim, Mohamed Omary, Maulid Tamila, Wilson Chigombo, Shaibu Mtita, Isack Emmanuel na Sheikhan Ibrahim aliyesajiliwa katika dirisha hili la usajili kutoka JKU
Kikosi hicho kimewajumuisha wachezaji 15 kutoka timu ya wakubwa ambao ni Aboutwalib Mshery, Chrispin Ngushi, Denis Nkane, Kibwana Shomari, Farid Musa na Clement Mzize
Pia wamo Zawadi Mauya, Jonas Mkude, Salum Abubakar, Skudu Makudubela, Fred Gifted, Jesus Moloko, Hafiz Konkoni, Joyce Lomalisa na Maxi Nzengeli
Yanga itashuka dimbani leo kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Jamhuri mchezo ukipigwa saa 2:15 usiku