JKT Tanzania imekuwa timu ya pili kutinga nusu fainali ya kombe la FA (ASFC) baada ya kuilaza Prisons mabao 2-0 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye dimba la Sokoine.
Licha ya kucheza kwenye dimba lake la nyumbani, maafande wa Prisons walijikuta wakichezeshwa kwata na maafande wa JKT ambao wamepanda daraja kushiriki ligi kuu msimu ujao.
JKT Tanzania imeungana na Stand United kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Azam FC na Mtibwa Sugar zitachuana kwenye dimba la Azam Complex Chamazi kwenye mchezo mwingine wa robo fainali wakati kesho Jumapili Singida United na Yanga zitachuana kwenye uwanja wa Namfua.

ADVERTISE HERE