Winga wa zamani wa Yanga Saimon Msuva anahusishwa tena kurejea kwa mabingwa hao wa nchi kwa awamu ya pili
Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi lakini Wananchi wanasubiri kukamilika kwa siku saba za ahadi iliyotolewa na Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ambapo baada ya siku hizo watatangaziwa mchezaji aliyesajiliwa
Lakini kama ni urejeo wa pili wa Msuva, ni wazi Wananchi wataupokea usajili huo kwa mikono miwili
Msuva amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya Taifa katika kipindi chote ambacho amecheza nje ya nchi
Huu utakuwa usajili wa ndani wenye thamani kubwa, kwa kuangalia uzoefu wake na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja
Msuva anaweza kutumika kama mshambuliaji, kiungo mshambuliaji au winga. Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kupachika mabao
Kwa idadi ya nafasi ambazo Yanga huwa wanatengeneza, kuwa na mchezaji aina ya Msuva pale mbele kutaongeza ufanisi katika matumizi ya nafasi
Msuva anaweza pia kutumika kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kama Yanga itatinga robo fainali
Alikuwa akiitumikia JS Kabylie ambayo haikuwa ikishiriki mashindano yoyote ya CAF