Wananchi wamemaliza kazi mkoani Dodoma kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United na sasa Wanarejea jijini Dar es salaam kuungana na familia zao katika shamra shamra za XMas
Mchezo dhidi ya Tabora United jana ulikuwa wa mwisho katika ligi kuu kwa mwaka 2023 Yanga ikifikisha alama 30 katika msimamo wa ligi alama moja nyuma ya Azam Fc inayoongoza ligi ikiwa na alama 31
Hata hivyo Yanga ina mechi mbili za viporo ambazo zitapangiwa tarehe baada ya michuano ya Afcon 2023 inayofanyika Ivory Coast kuanzia Januari 13 2024
Takribani wachezaji 13 wataelekea katika majukumu ya timu za Taifa kwa ajili ya maandalizi ya Afcon wakati wengine wataelekea Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
ADVERTISE HERE