Yanga imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu mkoani Dodoma baada ya kuichapa Tabora United bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Jamhuri
Bao pekee la Yanga katika mchezo huo lilipatikana kwenye kipindi cha kwanza kupitia mpira wa adhabu kutoka kwa Stephane Aziz Ki
Ulikuwa mchezo ambao Yanga ilihitaji matokeo ya ushindi zaidi ili kuendelea kuipa presha Azam Fc ambayo sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya alama moja lakini pia Yanga ikiwa na mechi mbili za viporo
Aziz Ki ameendelea kujichimbia juu katika orodha ya wafungaji akifikisha mabao 10
Yanga imefunga mwaka 2023 kwa ushindi muhimu





ADVERTISE HERE