Kikosi cha Yanga kiko mkoani Dodoma ambapo leo majira ya saa 1 usiku watashuka uwanja wa Jamhuri kuikabili Tabora United
Hii itakuwa mechi ya mwisho kwa mwaka 2023 katika ligi kuu baada ya Bodi ya Ligi kusogeza mbele mechi nyingine zilizopaswa kuchezwa tarehe 26 na 29
Alama tatu katika mchezo huo zitawahakikishia Wananchi kuendelea kusalia katika nafasi ya pili nyuma ya Azam Fc ambayo hata hivyo imecheza mechi tatu zaidi
Tabora United (zamani Kitayosce) na Yanga hazijawahi kukutana katika mchezo wowote na leo itakuwa mara ya kwanza
Yanga leo itaendelea kuwakosa Joyce Lomalisa ambaye ni majeruhi na Khalid Aucho anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu. Mchezo wa leo utakuwa wa pili
Hata hivyo kikosi cha kocha Miguel Gamondi kimesheheni mastaa wake wote muhimu na leo wamepania kuendeleza ubabe wao katika ligi kuu ya NBC msimu huu