Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo amedhamiria kupata ushindi wa kwanza katika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Saa 10 jioni Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Medeama Fc katika mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi
Baada ya kukosa ushindi katika mechi tatu zilizopita, hii ni nafasi nyingine kwa Gamondi kuwapa furaha Wananchi
Kikosi kitakachoshuka uwanjani leo pengine kinaweza kuwa na mabadiliko kulinganisha na kikosi alichotumia katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Al Ahly na Medeama ugenini
Gamondi leo huenda akarejea katika mfumo wake wa kutumia walinzi wanne badala ya watatu
Kuna uwezekano mkubwa Gamondi akarejea uwanja wa Benjamin Mkapa na kikosi alichotumia katika mchezo dhidi ya Simba na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1
Yanga leo inahitaji kucheza soka la kushambulia zaidi huku wakichukua tahadhari kwani Medeama watajilinda zaidi na kutumia mashambulizi ya kushitukiza
Hii ni mechi ambayo Medeama wanapaswa kukumbana na presha ya mashambulizi ndani ya uwanja na presha ya mashabiki majukwaani
Zaidi ya mashabiki 45,000 wanatarajiwa kuingia dimba la Mkapa kuipa sapoti Yanga