Tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Medeama - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2023
Tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Medeama - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanatambua kazi iliyo mbele yao katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama Fc ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi alisema wanahitaji kuweka hai matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata ya michuano hii hivyo wanahitaji ushindi

"Tumejiandaa vizuri kwa ajili huu mchezo muhimu sana kwetu, tunahitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata katika michuano hii"

"Tumekuwa na muda mzuri wa kufanya mazoezi, nawaamini wachezaji wangu, tutakuwa na mchezo mzuri dhidi ya Medeama hapo kesho,"alisema Gamondi

Gamondi amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao katika mchezo ambao wamedhamiria kushinda

"Mashabiki wa Yanga wamekuwa nasi kila hatua tangu mwanzoni mwa msimu, kesho ni mchezo muhimu tunawaomba waje kwa wingi, wachezaji wameahidi watafurahi baada ya dakika 90," aliongeza Gamondi

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage amesema wachezaji wote wako tayari na kila mmoja anafahamu alama tatu pekee zitawaweka katika nafasi nzuri katika kundi

"Sisi wachezaji tuko tayari, tunafahamu umuhimu wa mchezo huu, tunahitaji ushindi ili kuwa na matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata"

"Makocha wamefanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita hivyo tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Medeama hapo kesho," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’