Yanga vs Medeama; Jezi yako, tiketi yako

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2023
Yanga vs Medeama; Jezi yako, tiketi yako

Bilionea Ghalib Said Mohammed 'GSM' amelipa Tsh Milioni 225 kununua tiketi zote za Mzunguuko kwa ajili ya Wananchi kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumatano katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama Fc

Umuhimu wa mchezo huu umepelekea 'tajiri' kutoa fursa kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuwaongezea wachezaji wao hamasa katika mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi

Sasa kwa kuwa tiketi hizi ni kwa ajili ya mashabiki na Wanachama wa Yanga tu, Msemaji wa Yanga Ali Kamwe jana alitangaza utaratibu ambao utatumika kugawa tiketi hizo

Siku ya Jumatano, mageti ya uwanja wa Benjamin Mkapa yatafunguliwa saa 2 asubuhi ambapo utaratibu wa kugawa tiketi hizo utaanza muda huo

Sharti ili upate tiketi lazima uwe na jezi ya Yanga yenye nembo ya GSM. Jezi hiyo sio lazima iwe ya msimu huu, hata ikiwa ya misimu mitatu iliyopita ilimradi tu iwe imetengenezwa na GSM

Katika mchezo dhidi ya Al Ahly wengi wanakumbuka vurugu zilizotokea ambazo zilianzishwa na mashabiki waliokuwa kwenye jukwaa la Al Ahly lakini Yanga ilitakiwa kulipa gharama ya uharibifu uliojitokeza

Kama Yanga isingeweka sharti hili la jezi pengine mashabiki wa upande wa pili wangetumia fursa hiyo kuingia kwa wingi na yale yaliyojitokeza mchezo dhidi ya Al Ahly yakajitokeza tena

Kwa anayetaka kuingia uwanjani kupitia ofa ya GSM basi atapaswa kununua jezi kama sivyo akate tiketi za VIP A, B na C. Eneo la Mzunguuko ni maalum kwa ajili ya Wananchi tu

Shabiki ni mchezaji wa 12 uwanja, Yanga imeitumia silaha hiyo kikamilifu, ni suala la mashabiki kujitokeza kwa wingi kuhakikisha Medeama wanaziacha alama zote tatu Jumatano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’