Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi jana alikata kiu ya mashabiki waliokuwa na shauku ya kuwaona baadhi ya wachezaji ambao msimu huu wamekuwa na nafasi finyu ya kucheza
Ni katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulipigwa uwanja wa Azam Complex na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1
Gamondi aliwaanzisha Kibwana Shomari, Salum Abubakar 'Sure Boy', Jesus Moloko na Skudu. Wachezaji wote walikuwa na mchango katika ushindi huo
Kibwana alionyesha kiwango bora akitoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Stephane Aziz Ki wakati Moloko alitoa pasi ya bao la tatu lililofungwa na Kennedy Musonda huku Skudu akifunga bao la nne
Gamondi pia aliwapa nafasi wachezaji wengine katika kipindi cha pili Gift Fred, Farid Mussa na Crispine Ngushi wakiingia
Kama ni tuzo ya mchezaji bora wa mchezo, ukimtoa Aziz Ki aliyefunga mabao mawili, Sure boy ndiye mchezaji aliyen'gara zaidi na pengine anaweza kubadilisha mawazo ya Gamondi na kumpatia nafasi zaidi
Sure Boy alikuwa 'master' katika eneo la kiungo akikata umeme na kuanzisha mashambulizi. Haitakuwa ajabu kama Gamondi atamuanzisha kwenye mchezo dhidi ya Medeama
Kwa mara nyingine upana wa kikosi cha Yanga ulidhihiri katika ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar jana