Klabu ya Yanga leo itakuwa na Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Medeama ambao utapigwa Jumatano, Disemba 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. Mkutano huo utafanyika Salamanda Tower saa 6 mchana
Mchezo uliopita nyumbani katika ligi ya mabingwa alikabidhiwa 'afande' Ibrahim Bacca. Yanga inaendelea na utaratibu huo, leo atatangazwa mchezaji ambaye atabeba hamasa ya mchezo dhidi ya Medeama
Pia kumekuwa na tetesi kuwa tajiri GSM amenunua tiketi zote za mzunguuko lengo likiwa kuhakikisha Wananchi wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi
Ni saa sita mchana wa leo yote yatafahamika...!

ADVERTISE HERE