Yanga imebeba alama zote tatu uwanja wa Azam Complex baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 4-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Stephane Aziz Ki ameendeleza kasi yake ya kupachika mabao msimu huu akiweka kambani mabao mawili sasa akiongoza orodha ya wafungaji bora akifikisha mabao 9
Bao la kwanza alifunga kupitia mkwaju wa penati mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya Clement Mzize kuangushwa ndani ya eneo la hatari
Bao la pili alifunga katika kipindi cha pili akipokea pasi kutoka kwa Kibwana Shomari
Kennedy Musonda akafunga bao la tatu kwa guu la kushoto baada ya pasi ya kichwa kutoka kwa Jesus Moloko
Skudu leo amemtumia ujumbe kocha Miguel Gamondi kuwa anahitaji nafasi ya kucheza akionyesha kiwango akiifungia Yanga bao la nne
Bao la kufutia machozi kwa upande wa Mtibwa Sugar lilifungwa Seif Karihe katika mazingira ya utata kwani kabla ya kufunga alimfanyia madhambi Ibrahim Bacca akimpiga kiwiko na kumchana sehemu ya juu ya jicho
Ni ushindi muhimu kwa Yanga ambao unawasogeza karibu ya Azam Fc wakifikisha alama 27, alama moja nyuma ya Azam Fc ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi


