Dirisha dogo la usajili limefunguliwa leo Disemba 16 2023 na linatarajiwa kufungwa Januari 15 2024
Timu zinazoshiriki Ligi Kuu, Championship, First League na Ligi ya Wanawake zitakuwa na nafasi ya kufanya maboresho ya vikosi vyao
Pasipo na shaka Yanga itatumia kikamilifu dirisha hili kufanya maboresho katika maeneo yenye mapungufu
Utambulisho wa mchezaji wa kwanza aliyesajiliwa katika dirisha hili unatarajiwa kufanyika Azam Complex leo kabla ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa saa 12:30 jioni
ADVERTISE HERE