Klabu ya Yanga imemtambulisha mchambuzi wa video Mpho Maruping (32) raia wa Afrika Kusini
Kabla ya kujikita katika tasnia ya uchambuzi, Maruping alikuwa kiungo mahiri akicheza timu kadhaa ligi kuu ya Afrika Kusini
Aliachana na soka baada ya kupata majeraha yaliyomlazimu kugeukia majukumu mengine ya usimamizi wa soka
Ujio wake ni pendekezo la benchi la ufindi, Kocha Miguel Gamondi akihitaji mtaalam tofauti mwenye jukumu la kusoma wapinzani tu
Maruping amechukua nafasi iliyoachwa Khalil Ben Youssen ambaye aliondoka sambamba na kocha wa zamani wa Yanga Nasredine Nabi
Mtaalamu huyo alisoma masuala ya picha na video katika Chuo Kikuu cha Pretoria kabla ya kujikita zaidi katika uchambuzi wa mechi videoni na ukocha akianza kufanya kazi kama msaidizi wa Joel Masutha katika timu ya Pretoria Callies iliyokuwa Daraja la Pili (NFD).
Anaelezwa ni mtaalam wa kupanga mipango ya timu kuwasaidia makocha kupitia mechi mbalimbali za timu yake na hata wapinzani na alikuwa sehemu ya mafanikio ya timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini, Banyana Banyana iliyobeba ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Morocco.
Pia alikuwa kwenye kikosi kilichofika 16 Bora ya Fainali za Kombe la Dunia 2023 kwa kungβolewa na Uholanzi, huku akifanya kazi chini ya Akademi ya Rais wa sasa wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Dk Patrice Motsepe ya Venda Football Academy.