Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amesema wamejipanga kukabiliana na ratiba ngumu ya kufunga mwaka 2023
Katika mwezi Disemba 2023 Yanga ina ratiba ya mechi saba, mechi mbili tayari zimepigwa zikiwa zimebaki mechi tano
Mtine amesema pamoja na ugumu wa ratiba hiyo, wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri
"Tuna ratiba ngumu ya kucheza mfululizo mwezi huu Disemba lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri. Tunawaomba wanachama na Mashabiki wetu watuunge mkono ili kuhakikisha mkakati wetu wa kutetea ubingwa hautetereki"
"Tunaanza na Mtibwa Sugar Jumamosi, tunaomba mashabiki waje kwa wingi uwanja wa Azam Compex kutuunga mkono," alisema Mtine
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni Disemba 16 dhidi ya Mtibwa Sugar ukifuatiwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Medeama Fc Disemba 20
Disemba 23 Yanga itakuwa ugenini kuumana na Tabora United kisha kusafiri mkoani Kagera kuumana na Kagera Sugar Disemba 26
Disemba 29 Yanga itarejea Dar kuumana na Mashujaa Fc na kuukaribisha mwaka 2024 kwa mchezo mwingine nyumbani dhidi ya Dodoma Jiji Januari 02