Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Ngao ya Jamii kwa Wanawake umemalizika kwa Yanga Princess kuibuka na ushindi dhidi ya Fountain Gate Princess kupitia changamoto ya mikwaju ya penati
Ni baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana na Yanga Princess kushinda mikwaju ya penati 4-2
Yanga Princess sasa iko tayari kwa mikiki mikiki ya ligi kuu ya Wanawake inayoanza wiki ijayo
Hata hivyo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Haalubono ana kazi ya kuiboresha safu yake ya ushambuliaji kwani haijafunga bao katika dakika 180 walizocheza katika michuano hiyo
Kinadada hao Wananchi walipoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba Queens kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya 0-0
ADVERTISE HERE