Yanga inahusishwa kumuwania winga mahiri wa Fc Lupopo, Manu Lobota Bola kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo)
Baada ya usajili wa Maxi Nzengeli ambao umejibu haraka, mabosi wa Yanga wamerudi tena DR Congo na wanaweza kumshusha nchini Bola mbaye anatajwa kuwa winga hatari zaidi katika ligi kuu ya DR Congo kwa sasa
Ukaribu kati ya Mdhamini/Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohamed 'GSM' na Rais wa Fc Lupopo Jacques Kyabula Katwe unaweza kurahisisha ujio wa Bola ambao hata hivyo utamaanisha Yanga italazimika kuachana na nyota mmoja wa kigeni
Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Jumamosi, Disemba 16 ambapo Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa tayari anayo majina ya wachezaji waliosajiliwa, anasubiri dirisha lifunguliwe awatambulishe