Yanga Princess imetupwa nje ya Ngao ya Jamii baada ya kipigo cha mikwaju ya penati kutoka kwa watani zao Simba Queens katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana na hivyo mshindi kuamuliwa kwa mikwaju ya penati Simba Queens ikishinda 5-4

Yanga Princess itachuana na Fountain Gate Princess kusaka mshindi wa tatu
Fountain Gate Princess walichapwa mabao 5-0 dhidi ya JKT Queens katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali
ADVERTISE HERE