Maandalizi yanakwenda vizuri - Walter

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Dec 2023
Maandalizi yanakwenda vizuri - Walter

Meneja wa Yanga  Walter Harrison amesema timu inaendelea vyema na maandalizi katika Mji wa Kumasi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama Fc ambao utapigwa keshokutwa Ijumaa katika uwanja wa Baba Yara

Yanga ilitua Ghana jana na moja kwa moja kuanza mazoezi 'recovery', kikosi leo kinaendelea na program nyingine za mazoezi

Walter amesema mpaka sasa hawajakumbana na changamoto yoyote katika maandalizi ya mchezo huo

"Tunamshukuru Mungu tumesafiri salama kutoka Dar es salaam mpaka hapa Kumasi. Maandalizi yanaendelea vizuri jana tulikuwa na session maalum ya recovery ili kuondoa uchovu wa safari kwa wachezaji"

"Tumekuwa na mazoezi mengine ya recovery ya ndani na jioni tutafanya mazoezi ya uwanjani na tunatarajia program ya mwisho ya mazoezi tutaifanya kesho katika uwanja wa Baba Yara ambao utatumika siku ya mchezo"

"Hali ya timu kwa ujumla iko vizuri tunaushukuru uongozi wa Yanga kwa kuhakikisha tunafika hapa mapema na kupata muda wa kutosha kufanya maandalizi pamoja na kuzoea hali ya hewa," alisema Walter

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’