Yanga ilitua Ghana jana jioni na moja kwa moja kuunganisha kwenda Mji wa Kumasi ambao mchezo dhidi ya Medema utapigwa Ijumaa katika uwanja wa Baba Yara
Baada ya timu kuwasili Accra, ili kuwaepusha wachezaji na uchovu, uongozi wa Yanga ulikodi ndege binafsi iliyowapeleka Kumasi takribani kilomita 200 kutoka Accra
Yanga ikatumia chini ya dakika 45 mpaka Kumasi wakati kama wangechukua basi wangetumia takribani saa 4
Yanga imefikia hoteli ya kisasa ya Ridge Condos ambayo ndio hoteli ambayo inatumiwa na timu mbalimbali kubwa zinazofika kucheza hapo Kumasi
Wananchi wamepania kusaka ushindi dhidi ya Medeama ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za kuwania tiketi ya kufuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
ADVERTISE HERE