Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi said ambaye pia ni Mwenyekiti wa vilabu vya soka barani afrika (ACA), ametembelea eneo la mafuriko katika kijiji cha Katesh wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kutoa pole kwa waathirika wote wa mafuriko hayo
Akiunga mkono wito wa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na kwa kushirikiana na GSM Foundation Yanga ilichangia vitu vyenye thamani ya Tshs. 40,000,000 pamoja na fedha taslim Tshs. 10,000,000 kupitia Akaunti ya Mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa
Msaada huo ulipokewa na Mh. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akiambata na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Sendiga pamoja na viongozi mbalimbali walioko Katesh kusaidia zoezi zina la uokozi








ADVERTISE HERE