Mechi dhidi ya Medeama itakuwa kama fainali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2023
Mechi dhidi ya Medeama itakuwa kama fainali

Kikosi cha Yanga kimeondoka alfajiri ya leo kuwafuata Medeama SC, huku kocha mkuu Miguel Gamondi akiweka wazi kuwa dakika 180 za mechi mbili za kwanza zimempa mwanga kuelekea mchezo dhidi ya Medeama siku ya Ijumaa ambao utakuwa kama fainali

Akizungumza kabla ya kuondoka nchini, Gamondi alisema Yanga bado ina nafasi lakini wana kazi ya kuhakikisha wanajiandaa vyema ili kuendana na ushindani uliopo katika mechi zilizosalia

Gamondi amezitaja mechi mbili zilizopita dhidi ya CR Belouizdad na Al Ahly kuwa zimemsaidia kubaini mapungufu ya kikosi chake na ana matumaini watakuwa bora zaidi katika mchezo dhidi ya Medeama

"Makosa tuliyoyafanya hayawezi kujirudia tulikuwa bora dhidi ya CR Belouizdad tukapoteza kwa idadi kubwa ya mabao tukatulia na kusawazisha makosa kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly tumepata pointi moja. Mchezo unaofuata utakuwa mgumu lakini malengo ni pointi tatu," alisema

Gamondi amesema hakuna lisilowezekana kama watafanya maandalizi ya kutosha na kujiandaa vyema kuikabili Medeama, kila mchezo ulio mbele yao sasa ni fainali.

"Hatutakiwi kujiamini sana na kupelekea kufanya makosa kama tuliyofanya kwenye mechi mbili zilizopita. Naweza kukiri kuwa zimetupa darasa tutaingia kwenye mchezo ujao kwa tahadhari na kumuheshimu mpinzani"

"Hatua hii ni ngumu na kila timu ina malengo yake ya kuvuka hatua inayofuata, bado tuna nafasi ya kuvuka tukiwekeza nguvu huko na kuweka heshima mbele bila kujali tunakutana na nani" alisema Gamondi

Kikosi cha Yanga kimeondoka na msafara wa wachezaji 24 ambapo wanatarajiwa kutua Accra saa 10 jioni kisha kuunganisha kuelekea Mji wa Kumasi ambako mchezo dhidi ya Medeama utapigwa siku ya Ijumaa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’