Winga wa Yanga Maxi Nzengeli amesema wanakwenda Ghana kusaka alama tatu ili warejee katika malengo ya kufuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Maxi ambaye hakumaliza dakika zote 90 za mchezo dhidi ya Al Ahly, amesema hakuna nafasi ya kufanya makosa zaidi
Kiungo huyo mshambuliaji amekiri hakuwa katika ubora wake katika mchezo uliopita lakini ameahidi kupambana nchini Ghana katika mchezo dhidi ya Medeama
"Nimeumia kutokana na kushindwa kucheza vizuri kama ambavyo nilitaka nicheze lakini inatokea kwenye soka hatujakata tamaa bado akili yetu ipo kamili"
"Tunarudi kwa nguvu mechi ijayo, haitajalisha tupo ugenini tutaenda kutafuta ushindi ili kurudi kwenye malengo"
"Kila mchezaji anataka kuona Yanga ikivuka kwenda robo na hii haiwezekani kama hatutapambana. Tupo tayari na tunaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono," alisema Maxi