Tulihitaji ushindi dhidi ya Al Ahly - Pacome

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Dec 2023
Tulihitaji ushindi dhidi ya Al Ahly - Pacome

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amesema hayakuwa malengo yao kutoka sare dhidi ya Al Ahly kwani walihitaji kushinda mchezo huo wa kwanza nyumbani

Hata hivyo Pacome amesema wameipokea alama hiyo moja na sasa wanajipanga kuhakikisha wanashinda mchezo unaofuata dhidi ya Medeama

"Yote anapanga mungu tutarejea katika wimbi la ushindi katika mechi zijazo. Nawapongeza wachezaji wenzangu kwa mchezo mzuri"

"Nafurahi kufunga bao langu la kwanza kwenye hatua ya makundi ligi ya mabingwa," alisema Pacome

Bao la Pacome alilofunga dakika 90 liliihakikishia Yanga kupata alama moja dhidi ya Al Ahly waliotangulia kufunga bao kwenye dakika ya 87 kupitia kwa Pecy Tau

Pacome alikuwa bora katika mchezo huo, amestahili tuzo ya mchezaji bora wa mechi  iliyopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’