Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika ambaye pia anaongoza Kamati ya Mashindano, amesema Yanga haijawahi kuzungumza na kiungo wa Singida United Mudathir Yahya juu ya kumsajili.
Kumekuwa na taarifa kwamba Yanga imeanza mchakato wa kunasa sahihi kiungo huyo ambaye mkataba wake wa kuitumikia Azam FC umemalizika juzi.
Imeelezwa kuwa Mudathir aligoma kusaini mkataba mpya na Azam FC hivyo kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mktaba wake kumalizika.
Nyika amesisitiza kwamba huu sio wakati wa kuzungumzia maswala ya usajili, mawazo ya Yanga yako kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Singida United April 01.
Muthadir amekuwa katika kiwango bora tangu ajiunge na Singida United akitolewa kwa mkopo na Azam FC.

ADVERTISE HERE