Mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Ulikuwa mchezo uliojaa mbinu nyingi kutoka kwa kila upande, mabao yakipatikana dakika za lala salama
Pecy Tatu alifunga bao la Al Ahly dakika ya 88 akitumia makosa yaliyofanywa na nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto
Hata hivyo dakika mbili baadae Pacome Zouzoua aliisawazishia Yanga kwa bao la shuti kali akipokea pasi kutoka kwa Kennedy Musonda
Ni alama moja muhimu kwa Yanga pamoja na kuwa ushindi nyumbani ndio matokeo muhimu zaidi ambayo Yanga ilihitaji
Mchezo unaofuata Disemba 09 ni dhidi ya Medeama Fc huko Ghana




ADVERTISE HERE