Hamasa kwa mashabiki wa Yanga ni kubwa kuelekea kilele cha Bacca Day, Disemba 02 kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe ameendelea na hamasa jijini Dar ambapo muitikio wa Wananchi ni mkubwa
Ni siku mbili tu zimesalia, Benjamin Mkapa itakuwa 'full house', kama bado hujakata tiketi basi una siku ya Ijumaa kuhakikisha umeikamata tiketi yako
Kuna mabasi kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Arusha, Dodoma, Kilimanjaro na maeneo mengine yataleta mashabiki kwa maelfu
Jijini Dar es salaam inaelezwa misuli imekuwa adimu madukani! Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani Wananchi wamehamasika na wamejiandaa kumuheshimisha Bacca Jumamosi
Wakati maandalizi ya nje ya uwanja 'yakinoga', Kocha Miguel Gamondi yeye anaendelea kukiandaa kikosi Avic Town
Utaratibu ambao Yanga inatumia kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly, hautofautiani na utaratibu ambayo Yanga ilijiandaa kabla ya mchezo dhidi ya Simba
Ukimya ametawala Avic Town, mazoezi yanaendelea chini ya ulinzi mkali, Jumamosi Al Ahly watakutana na wasichotarajia...!









