Mwasisi wa kionjo cha Tabu lele laaah... kilichotumiwa na Yanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba, anatarajiwa kuwasili leo akitokea DR Congo
Tabu lele.. laah.. ni msemo uliopata umaarufu miongoni mwa mashabiki wa Yanga hasa baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya watani zao Simba
Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema 'mwamba' huyo atawasili JNIA saa 4 usiku akiwataka mashabiki wa Yanga kwenda kumpokea
Kamwe amesema msanii huyo atashirikiana na msanii mkubwa hapa Tanzania (hakutaja jina) kurekodi tabulele na kufanya kuwa wimbo rasmi wa hamasa
"Tabulele atakuwepo Jumamosi kuwapa burudani mashabiki wa Yanga kabla ya mchezo dhidi ya Al Ahly. Niaambie tu, atawasili nchini hii leo saa 4 usiku. Kwa wale wtakaokuwa na nafasi tujitokeze JNIA kwani tabulele itaanzia hapo hapo uwanja wa ndege"
"Baadae Tabulele ataelekea moja kwa moja studio kurekodi wimbo huo akishirikiana na msanii mkubwa kutoka hapa nchini. Tunataka kuifanya hii Tabulele uwe wimbo wetu wa hamasal," alisema Kamwe