Wapinzani wa Yanga katika mchezo wa ligi ya mabingwa, Al Ahly wanatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi kuelekea mchezo kati ya timu hizo ambao utapigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Al Ahly leo wanatarajiwa kucheza mechi ya ligi kuu dhidi ya Smouha kabla kuianza safari ya kuja Tanzania siku ya Alhamisi
Utakuwa mchezo wa pili kundi D Yanga ikihitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele hatua ya robo fainali
Al Ahly wanaongoza kundi D kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Medeama wakiwa sawa na CR Belouizdad ambayo iliichapa Yanga mabao 3-0 pia
ADVERTISE HERE