Jana kikosi cha Yanga kilianza maandalizi ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Jumamosi, Disemba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad uliopigwa ugenini, Yanga inahitaji kuzibakisha alama zote tatu nyumbani kwa kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi kina nafasi ya kushinda mchezo huo na malengo yake ni kuona Yanga inatinga robo fainali
"Mchezo uliopita umekuwa darasa hatutaki kurudia tena makosa tunahitaji kutumia vyema uwanja wetu wa nyumbani kwa lengo la kuhakikisha tunarudi kwenye ushindani japo haitakuwa rahisi"
"Kuna kazi kubwa inahitajika kufanyika kwa wachezaji wangu ili tuweze kupata matokeo nyumbani naamini hilo litafanikiwa kutokana na maelekezo ya kiufundi niliyo wapatia"
"Malengo yetu ni kusonga hatua inayofuata na hilo naamini litawezekana kama wachezaji wangu watacheza kwa malengo na ushindani"
"Kukosa matokeo kwenye mchezo wa kwanza haiwezi kuwa sababu ya kutukatisha tamaa bado tuna nafasi ya kufanya vizuri hasa tukianza na matokeo mazuri nyumbani," alisema Gamondi