Juzi Asec Mimosas walikuwa nchini kuchuana na Simba katika mchezo wa ligi ya mabingwa uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Asec walisawazisha bao kwenye kipindi cha pili kupitia kwa Serge Pokou baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Sankara Karamoto aliyetoa pasi ya bao hilo
Akiwa na umri wa miaka 20 tu, Karamoko ni mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Asec
Mara ya baada ya mchezo juzi, harakati za kumnasa kinda huyo anayeweza kutumika katika eneo la ushambuliaji na winga, zikagonganisha Yanga, Simba na Azam Fc
Lakini iko wazi kama Sankara atakuja kucheza Tanzania ataichagua timu moja tu. Yanga ina nyota watatu kutoka Asec wawili wakisajiliwa katika dirisha lililopita
Hapa tunawazungumzia Stephane Aziz Ki, Yao Kouassi na Pacome Zouzoua. Yanga ina mahusiano mazuri na Asec hivyo haitakuwa kazi kubwa kwa Injinia Hersi Said kumnasa Karamoko
Hata hivyo kama Yanga itamsajili Karamoko ni wazi itakuwa kwa ajili ya msimu ujao. AKitua dirisha dogo anaweza kutumika kwenye mashindano ya ndani tu kwani tayari ameitumikia Asec kwenye ligi ya mabingwa