Wachezaji wanne kati ya watano waliokuwa kwenye kikosi cha Stars kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo na kupata ushindi wa mabao 2-0 jana, wamewasili kwenye kambi ya Yanga mkoani Morogoro.
Gadiel Michael, Hassani Kessy, Kelvin Yondani na Ibrahim Ajib pamoja na kocha msaidizi Noel Mwandila wamesafiri mchana wa leo kujiunga na kikosi cha Yanga mkoani Morogoro.
Mlinda lango Ramadhani Kabwili amebaki jijini Dar es salaam kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 inayojiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON kwa vijana March 31.
Kabwili ameunga na wachezaji wengine wawili wa Yanga Maka Edward na Said Mussa 'Ronaldo' walio kwenye kikosi hicho cha Ngorongoro Heroes.

ADVERTISE HERE