Tulipoteza mchezo sio malengo - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2023
Tulipoteza mchezo sio malengo - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kimepoteza mchezo dhidi ya CR Belouizdad lakini hawajapoteza malengo yao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Yanga ilirejea nchini Alfajiri ya leo wakitokea Algeria ambako walipoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kwa kufungwa na CR Belouizdad mabao 3-0 

Gamondi amesema pamoja na vijana wake kucheza vizuri mchezo huo, walifanya makosa matatu ambayo yaliwanufaisha wapinzani wao

"Tulifanya makosa makubwa matatu, nadhani ndio hayo ambayo yamewapa ushindi wenzetu, ni makosa ya kushindwa kucheza kwa nidhamu ya mchezo, hayo ndiyo matokeo ya soka wakati mwingine unaweza kucheza vizuri lakini matokeo akapata mpinzani"

"Hatuna muda wa kupoteza, tunarudi kujiandaa na mchezo ujao, tutakwenda kukutana na timu nyingine bora, hatuna budi kusahau yote ya mchezo huu kwani ile ni mechi nyingine dhidi ya timu nyingine"

"Tunarudi moja kwa moja kambini kuanza maandalizi, hakutakuwa na muda wa kupumzika, tumezungumza na wachezaji tutarudi eneo la mazoezi kujipanga ili makosa kama haya yasijirudie," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’