Aziz Ki aiwahi CR Belouizdad

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Nov 2023
Aziz Ki aiwahi CR Belouizdad

Stephane Aziz Ki msimu huu nyota yake inan'gara kwelikweli katika klabu ya Yanga, anafunga vile atakavyo na kutengeneza mabao kwa wengine

Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji ambao ni gumzo katika jiji la Algiers kuelekea mchezo wa kesho sambamba na Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli ambao wanaunda pacha iliyopewa jina la MAP

Aziz Ki alitua Algiers jana baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa Burkina Faso

Wachezaji wengine walioingia Algeria jana ni pamoja na mlinda lango Djigu Diarra na kiungo Khalid Aucho

Wengine ni Metacha Mnata, Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ibrahim Bacca, bakari Mwamnyeto. Mudathir Yahya na Clement Mzize waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Kikosi cha Yanga leo kitafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa July 05 ambao mchezo dhidi ya CR Belouizdad utapigwa kesho saa 4 usiku

Ni katika uwanja uleule ambao Yanga iliichapa USM Alger bao 1-0 katika mchezo wa pili wa fainali kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’